Kuelekea Sayuni - movie trailer in swahili language

Video

April 16, 2015

Zaidi ya miaka 4,000 iliyopita, Mungu alimjia Abraham huko Mesopotamia na kumwaagiza, " Ondoka katika nchi yako, waache watu wako na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha. Mimi nitakufanya taifa kubwa na nitakubariki." Abraham akatii maagizo ya Bwana na akaenda kwenye nchi ya ahadi ambapo aliishi yeye na mwanawe Isaka na mjukuu wake Yakobo, ambaye baadaye aliitwa "Israeli."

Israeli na wanawe 12 walielekea Misri kwa sababu ya njaa iliyofika nchi ya Kanaani na huko wakazaana na kuwa taifa kubwa. Wamisri walishikwa na hofu kwa sabubu ya taifa kubwa la Israeli kuishi miongoni mwao – basi wakawafanya watumwa na kufanya maisha yao kuwa ya dhiki kwa utumwa usiomithilika. Baada ya miaka 430 nchini Misri, waliokolewa na Musa kutoka mateso ya utumwa, wakavuka Bahari ya Shamu na kuingia Arabia walikopokea amri kumi katika Mlima wa Sinai.

Kile kizazi cha Waisraeli waliotoka Misri na Musa hakikuruhusiwa kuingia kwenye Nchi ya Ahadi kwa sababu walikosa imani kwa Bwana. Walilazimika kuzunguka jangwani kwa miaka 40 mpaka kizazi kingine kikakua – kilichomtumainia Bwana nacho kikaingia nchi ya ahadi na Joshua.

Kwa takribani miaka 400, makabila 12 ya Israeli yalitawaliwa na Waamuzi kwa mujibu wa sheria za Musa. Walipotamani wawe na mfalme kama mataifa mengine, Mungu akamteua Sauli awe mfalme wao, naye akawatawala kwa miaka 40, akafuatwa na Mfalme Daudi – aliyetawala kwa miaka 40, na Sulemani mwana wa Daudi, aliyetawala kwa miaka 40. Ni katika kipindi cha Sulemani ambapo ufalme wa Israeli ulitukuka zaidi, na hekalu la kwanza likajengwa; lakini kwa sababu moyo wa Sulemani ulimuasi Bwana katika umri wake wa uzee, Mungu akamwambia kuwa makabila 10 hayatatawaliwa na mwanawe.

Baada ya kifo cha Sulemani, ufalme wa Israeli ukatawanyika, na makabila 10 ya kaskazini yakatawaliwa na msururu wa wafalme waovu ambao hawakuwa wa uzao wa Daudi na Sulemani. Ufalme huo wa Kaskazini ulihifadhi jina la Israeli na hatimaye kulifanya jiji la Samaria makao yake makuu. Ufalme mdogo wa Kusini ukaitwa Yuda na kuwa na Yerusalemu kama makao yake makuu; nao ukatawaliwa na kizazi cha Daudi. Kuanzia 2 Wafalme 16, watu wa Ufalme wa Kusini walikuja kujulikana kama "Wayahudi" kutoka na ufalme wa Yuda.

Kwa sababu ya uovu wa Ufalme wa Kaskazini ya Israeli, waling'olewa na kufanywa mateka na Waashuri. Waisraeli waliobaki waliingiliana na watu wa mataifa waliokuja kukaa kwenye nchi. Hawa ndio waliokuja kufahamika kama Wasamaria, na yale makabila 10 ya Israeli Kasikazini yasiweze kuwa taifa tena.

Nao Ufalme wa Kusini wa Yuda hatimaye ukapelekwa mateka huko Babiloni kama adhabu ya kutumikia miungu mingine na hekalu likabomolewa, ingawa baada ya miaka 70, Wayahudi walirejea Yuda, wakajenga lile hekalu tena na kuendelea kutawaliwa na wafalme wa kizazi cha Daudi.

Katika kipindi cha Kristo, taifa la Yuda lilikuwa linafahamika kama Judea na lilikuwa chini ya utawala wa Kirumi. Yesu Kristo na wanafunzi wake walihubiri injili kote Judea wakitafuta kondoo wapotevu kwenye nyumba ya Israeli. Baada ya miaka 3 na nusu ya huduma, Wayahudi walimkana Yesu kama mkombozi wao na kumshawishi gavana wa Kirumi kumsulubisha. Siku 3 baadaye, akafufuka na kujitambulisha mbele ya wanafunzi wake kabla hajapaa na kuketi kwenye mkono wa kulia wa Baba mbinguni.

Kabla hajasulubiwa, Yesu alitabiri kuwa adhabu ya kumkana, ni Yerusalemu kuteketezwa, hekalu kuharibiwa, na Wayahudi kutawanyika kwa mataifa yote. Utabiri huu ulitimia mwaka wa 70 A.D. wakati mfalme wa baadaye wa Kirumi, Tito, alivamia na kushinda Yerusalem. Kwa zaidi ya miaka 1800, Wayahudi wakawa wametawanyika kwa mataifa yote.

Halafu mawaka wa 1948, kisichofikirika kikafanyika. Nchi huru ya Israeli ikaanzishwa, na Wayahudi kwa mara nyingine wakamiliki nchi ya ahadi. Wakristu wengi wametangaza jambo hili kama muujiza na baraka toka kwa Mungu, lakini je, hii ilikuwa baraka toka kwa Bwana au nguvu za giza zilihusishwa? Filamu hii ina jibu.

 

 

 

mouseover